KIMBUNGA MAREKANI : WATU 18 WAUAWA GEORGIA NA MISSISSIPPI - Rhevan Media

KIMBUNGA MAREKANI : WATU 18 WAUAWA GEORGIA NA MISSISSIPPI

MississippiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWatu wanne wameuawa na kimbunga kusini mwa Mississippi
Watu zaidi ya 18 wamefariki kutokana na kimbunga kikali na hali mbaya ya hewa kusini mwa Marekani, maafisa wa uokoaji wamesema.
Watu wengi wamejeruhiwa. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni majimbo ya Georgia na Mississippi.
Gavana wa Nathan Deal ametangaza hali ya tahadhari katika wilaya saba kusini na katikati mwa Georgia ambapo watu 14 wamefariki.
Watu wanne waliuawa na vimbunga Mississippi siku ya Jumamosi.
Bado kuna hatari ya kimbunga kupiga maeneo ya kusini mwa Florida, idara ya taifa ya hali ya hewa imeonya.
Idara ya huduma za dharura ya Georgia imesema watu 14 walifariki katika wilaya za Cook, Brooks, Dougherty na Berrien katika jimbo la Georgia.
Vifusi Adel, Georgia, U.S. Januari 22, 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaeneo ya Adel, Georgia, yaliathiriwa sana na kimbunga
Nyumba nyingi zimebomolewa katika wilaya ya Cook.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema amewasiliana na Gavana Deal na kumpa salamu za rambirambi kutokana na vifo vilivyotokea.
Kusini mwa Mississippi, watu wanne walifariki kutokana na kimbunga ambacho kilikuwa na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi ya 218 km/h (136 mph).
Watu zaidi 50 walijeruhiwa.
A house severely damaged by a tornado in Mississippi on 21 January 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionThe violent storms have also damaged property
Map of Georgia

Mada zinazohusiana

Previous
Next Post »