KIMAIRA : WANAYANSI WAFANYA JARIBIO LA HATARI ZAIDI DUNIANI BAADA YA KUFANYA HILI TUKIO KWA NGURUWA NA BINADAMU - Rhevan Media

KIMAIRA : WANAYANSI WAFANYA JARIBIO LA HATARI ZAIDI DUNIANI BAADA YA KUFANYA HILI TUKIO KWA NGURUWA NA BINADAMU

KiiniteteHaki miliki ya pichaJUAN CARLOS IZPISUA BELMONTE
Image captionViinitete hivyo vilikua kwa siku 28
Viini tete ambavyo ni 0.001% binadamu na sehemu iliyosalia ni nguruwe, vimekuzwa na wanasayansi nchini Marekani.
Hicho ni kisa cha kwanza kwa viumbe ambao ni mseto wa binadamu na viumbe wengine kuzalishwa kwa kuunganisha sehemu kutoka kwa binadamu na viumbe vingine.
Lengo limekuwa kujaribu kubaini iwapo inawezekana viungo vya binadamu kukuzwa kwenye wanyama.
Hata hivyo, makala ya kisayansi iliyoandikwa kwenye jarida la Cell inaonyesha shughuli hiyo ina changamoto nyingi.
Makala hiyo imeelezwa kuwa "ya kusisimua sana" na watafiti wengine.
Ilii kuunda kiini tete kama hicho ambacho kimepewa jina kimaira (Chimera), - ambaye ni mnyama katika hadithi mwenye kichwa cha simba, mwili wa mbuzi na mkia wa nyoka, atokaye moto kinywani - wataalamu walitumia seli tete (seli zinazoweza kukua kuwa seli za aina yoyote mwilini) na kuziweka ndani ya kiini tete cha nguruwe.
SeliHaki miliki ya pichaJUAN CARLOS IZPISUA BELMONTE
Image captionKiini tete cha nguruwe kiliongezwa seli za binadamu
Kiini tete hicho - ambacho sasa kimechanganyikana seli za binadamu na nguruwe - kiliwekwa ndani ya nyumba ya uzazi ya nguruwe jike na kukaa kwa mwezi mmoja.
Shughuli hiyo hata hivyo ilikuwa na changamoto nyingi na kati ya viini tete 2,075 vilivyowekwa ndani ya nguruwe, ni viinitete 186 vilivyokuwa hadi siku ya 28.
Hata hivyo, kulikuwa na dalili za matumaini kwamba seli za binadamu zilikuwa bado zinakuwa, ingawa ziliunda sehemu ndogo sana ya viungo vya mwili kwenye kiinitete hicho kilichochanganyikana seli za nguruwe na binadamu.
"Hii ndiyo mara ya kwanza kwa seli za binadamu kuonekana zikikua ndani ya mnayama mkubwa," Prof Juan Carlos Izpisua Belmonte, kutoka taasisi ya Salk, ameambia BBC.
Seli za binadamu na nguruweHaki miliki ya pichaJUAN CARLOS IZPISUA BELMONTE
Image captionSeli za binadamu, zenye rangi ya kijani, zikionekana ndani ya kiinitete cha wiki nne
Wataalamu hao wa Salk wanasema viinitete vya kimaira vinaweza kutumiwa:
  • kufanyia majaribio dawa kabla ya majaribio kwenye binadamu
  • kuchunguza chanzo cha magonjwa ya binadamu
  • kufahamu zaidi ukaji wa viinitete vya dinadamu.
  • kufafanua tofauti kati ya viungo vya viumbe tofauti
ChimeraHaki miliki ya pichaTHINKSTOCK
Image captionChimera ni mnyama katika hadithi za Ugiriki mwenye kichwa cha simba, mwili wa mbuzi na mkia wa nyoka, atokaye moto kinywani

Mada zinazohusiana

Previous
Next Post »