KAIRUKI NAYE ATANGAZA SAFARI YAKE YA DODOMA - Rhevan Media

KAIRUKI NAYE ATANGAZA SAFARI YAKE YA DODOMA


Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi ya Umma na Utawala bora imehamia Makao Makuu ya nchi Jijini Dodoma ikiwa ni siku chache baada ya agizo lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu la kuzikumbushia wizara zote kuhamia mkoani humo ifikapo Februari 28.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofis
Akizindua safari ya kwanza ya Wizara hiyo, hii leo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki amesema, kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.
"Leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde (Leo) vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”, Amesema Mhe. Kairuki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi
Aidha, amesema kwa mahitaji na ofisi hiyo ikiwa pamoja na kukutana na waziri kuhusu masuala sera na sheria za utumishi wa umma na utawala wa utumishi wa umma yatatekelezwa katika ofisi za Dodoma zilizopo katika jengo la College of Hummanities and Social Sciences ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma mkoani humo.
Previous
Next Post »