ISRAEL YAISHUTUMU IRAN KWA KUJARIBU KOMBORA LAKE - Rhevan Media

ISRAEL YAISHUTUMU IRAN KWA KUJARIBU KOMBORA LAKE

Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri
Image captionIsrael imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri
Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri
Waziri mkuu nchini humo Benjamin Netanyahu amesema kuwa jaribio hilo la kombora la masafa ya kadri ni ukiukaji wa sheria za Umoja wa Mataifa.
Amesema kuwa atapigania Iran kuwekewa vikwazo vipya vya kimataifa wakati wa ziara yake mjini Washington mwezi ujao.
Maafisa wa Marekani wamethibitisha kufanyika kwa jaribio hilo la kombora lakini wakasema kuwa haijabainika iwapo lilikiuka sheria za Umoja wa Mataifa iliopitishwa 2015 kufuatia mpango wa kimataifa kuuwekea vikwazo mpango wa Nuklia wa Iran.
Hakujakuwa na tamko lolote kutoka Iran.
Kabla ya kuchukua mamlaka ,rais Trump alitaja mpango huo wa Iran kuwa hatari 
Previous
Next Post »