Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni vyema wananchi wakaanza kuwapuuza
wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakigeuza matatizo ya
wananchi kama mtaji wa kisiasa.
Hayo
yamesemwa na katibu wa Siasa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey
Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.
“CCM
haitashiriki malumbano yasiyo kuwa na tija kwa lengo la kuleta
uchochezi kwa wananchi kama ilivyo kwa viongozi wa vyama vya upinzani
nchini, ambao wamekuwa wakitoa matamko kuwa Taifa limekumbwa na baa la
njaa kama sehemu yao ya mtaji wa kisiasa, jambo ambalo Chama cha
Mapinduzi kinaona hiyo ni siasa chafu” amesema Polepole.
Amesema
kuwa kwanza tuwapuuze na maneno yao, kwani mwenye mamlaka ya kutangaza
baa la njaa nchini ni Rais peke yake, hivyo ni vema wakajua kuwa
Tanzania hatujafikia kiwango hicho, ambao wao wanakiomba, bali
wanatakiwa kujua kuwa mpaka sasa tuna kiasi cha Tani Milioni 1 na nusu
ambacho kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ambayo yana upungufu wa
chakula.
Ameongeza
kuwa sera ya CCM ni kujitegemea, hivyo kama ndicho chama ambacho
kinaongoza dola,hatujafikia hatua ya kukosa chakula katika nchi yetu.
Pole Pole Ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha kubweteka na kuwalaghai na kuwafarakanisha Wananchi,bali
wanapaswa kuwaambia ukweli wananchi ili waweze kutunza nafaka na kuacha
kutumia kwa matumizi mabaya kama kupikia pombe na masuala mengine
yasiyokuwa ya lazima.
Sign up here with your email