Taarifa kutoka
katika Ikulu ya Marekani zinaeleza kuwa , inaonekana kwamba wafungwa
zaidi kutoka katika gereza la Guantanamo Bay walioko kizuizini
wanatarajiwa kuachiliwa kabla rais Barack Obama hajaondoka rasmi
madarakani mpaka kufikia tarehe ishirini ya mwezi huu.
Rais Obama
amesema kuifunga kambi hiyo ndiyo kipaumbele chake miaka nane iliyopita
wakati alipokuwa akiingia madarakani, akitilia mkazo maelezo hayo
ameongeza kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa gereza hilo kuna shusha
hadhi ya wamarekani.Akiieleze kambi hiyo amesema kwamba imekuwa eneo la mashaka, kushikiliwa kwa muda mrefu, kulazimishwa kula chini ya ulinzi , kunyimwa usingizi, nafasi ya dhiki, vipigo visivyokwisha , na aina nyingine ya mateso tele.
Hata hivyo idadi ya wafungwa imekuwa ikipungua kila uchao, na mpango wa kuifunga kambi hiyo ya mateso umekuwa ukipingwa na bunge la Congress.
Naye rais mteule wa Marekani Donald Trump, ametanabahisha dhahiri msimamo wake na kupinga wazo la kumuachilia mfungwa yeyote kutoka katika gereza hilo. Akiweka bayana msimamo huo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter amesema kwamba wafungwa hao ni watu hatari na hawana ruhusa ya kurejea katika uwanja wa vita.
Sign up here with your email