BAD NEWS : MOTO WA NYIKA WAANGAMIZA MJI CHILE - Rhevan Media

BAD NEWS : MOTO WA NYIKA WAANGAMIZA MJI CHILE

Santa OlgaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMjini Santa Olga, nyumba 1,000 zimeteketea kabisa
Mataifa yameanza kutuma wazima moto nchini Chile kusaidia taifa hilo kukabiliana na moto mbaya zaidi katika historia ya taifa hilo.
Urusi imetuma ndege yenye uwezo wa kubeba tani kadha za maji kujaribu kusaidia kuzima moto huo wa nyika.
Moto huo umeenea kwa kasi sana maeneo ya kati ya Chile, ambapo unasaidiwa na upepo mkali, kiwango cha juu cha joto na hali kwamba maeneo hayo yamekabiliwa na kiangazi kwa muda.
Mji Santa Olga, unaopatikana kilomita 240 kusini mwa Santiago umeharibiwa kabisa na moto huo.
Santa Olga, 240Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMwiili wa mtu mmoja uliokuwa umeteketea ulipatikana katika mji wa Santa Olga. Watu 6,000 walifanikiwa kutoroka bila majeraha.
San RamonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWakazi walitoroka wakiwa na wanyama wao. Hapa, wakazi wanaonekana ndani ya gari, farasi wao akikimbia kuandamana nao nje
Santa Olga, 26 Januari 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu wengi wameacha bila makao na bila matumaini
Chile. 26 Januari 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMoto huo umeteketeza karibu hektari 238,000 (ekari 588,000) kote nchini Chile. Maafisa wa msitu wanasema moto huo unaendelea kuenea
Llico, 26 Januari 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWazima moto wamekuwa wakiombolewa wenzao watano waliofariki wakikabiliana na moto huo na kuwaokoa wakazi

Mada zinazohusiana

Previous
Next Post »