AL-SHABAB WASHAMBULIA HOTELI MOGADISHU - Rhevan Media

AL-SHABAB WASHAMBULIA HOTELI MOGADISHU


Wapiganaji wa al-ShababHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKundi la al-Shabab limekiri kuhusika
Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanachama wa al-Shabab wameshambulia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Watu hao wenye silaha wameingia kwenye hoteli hiyo baada ya kulipuliwa kwa mabomu mawili kwenye lango la kuingia kwenye hoteli hiyo.
Kapteni Mohamed Hussein wa kikosi cha polisi nchini humo ameambia wanahabari kwamba watu wengi, wakiwemo wanasiasa walikuwa kwenye hoteli hiyo ya Dayah.
Amesema ufyatulianaji mkali wa risasi bado unaendelea ndani ya hoteli hiyo.
Idadi kamili ya waliouawa pamoja na majeruhi haijabainika.
Kundi la al-Shabab limekiri kuhusika.
Previous
Next Post »