AGIZO LA JPM KWA WAZIRI SIMBACHAWENE NA PROF. MBARAWA LAKOSA MAJIBU - Rhevan Media

AGIZO LA JPM KWA WAZIRI SIMBACHAWENE NA PROF. MBARAWA LAKOSA MAJIBU

Tokeo la picha la rais jpm

iwa imepita siku moja tangu Rais John Pombe Magufuli kuwaagiza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene kutoa taarifa za faida iliyozalishwa na mradi wa mabasi yaendayo haraka tangu ulivyoanza mwezi Mei, 2016 hadi sasa.
Leo Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amefafanua jumla ya mapato yaliyozalishwa na kusema kuwa faida halisi itafahamika pindi wadau wa mradi huo watakapo ainisha matumizi ya mradi huo tangu ulipoanza.
“Kujua faida halisi ni suala la kukaa chini na kutathimini makusanyo pamoja na uainishwaji wa matumizi tangu ulipoanza,” amesema.
Amesema kuwa, mapato ya mradi huo ambao ulikuwa katika uendeshwaji wa mpito yalikuwa yanaongezeka kila mwezi kutoka milioni 800 mwezi Mei hadi Bilioni 3.3 Disemba na kwamba jumla ya makusanyo tangu ulipoanza ni zaidi ya bilioni 19.
Ameeleza kuwa, kutokana na mapato yake kupanda, endapo matumizi yatadhibitiwa  utajiendesha kwa faida pamoja na serikali kupata gawiwo lake kwa wakati.
Hata hivyo, amesema serikali itaendelea kunufaika na mradi huo hususan kwamba itapokea gawiwo la faida mara mbili ikiwemo kupitia hisa zake asilimia 49 za UDART.
“Mradi huu unaendelea vizuri kwa kuwa upo katika uendeshaji wa mpito na kwamba ni sehemu yetu ya majaribio ya mradi ambapo mapato yamekuwa yakiongezeka kila mwezi kuanzia milioni 800, hadi bilioni 3.3 kila mwezi,”amesema.
“Biashara inayoweza kujilipia gharama zake za uendeshaji ukiudhibiti vizuri mahali fulani unaweza pata faida nzuri na serikali kupata gawiwo lake,” amesema.
Previous
Next Post »