Utani ukizidi ni
shida, kwani Yanga ilipanga kuondoka leo saa 1:00 asubuhi kwenda
Zanzibar, lakini imelazimika kufuta safari yake baada ya kubaini
wangepanda boti moja na Simba katika safari yao.
Timu zote hizo
zinakwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo
imeanza jana Ijumaa usiku kwa kushirikisha timu za Zanzibar, Tanzania
Bara na Uganda.
Mchezo ulikuwa hivi,
Yanga ilikatiwa tiketi ya boti ya Kilimanjaro kwenda Zanzibar leo saa
1:00 asubuhi, walipododosa wakabaini katika boti hiyo pia kikosi cha
Simba kitakuwemo.
Kuona hivyo, viongozi
wa Yanga wakalazimika kubadili tiketi za timu yao na kusogeza muda hadi
saa 9:00 alasiri watakapoanza safari lengo likiwa ni kutopanda boti
moja na Simba.
Mmoja wa viongozi wa
Yanga, alilithibitishia Championi Jumamosi kuhusu hali hiyo na kusema
sasa kila kitu kipo sawa na wao watapanda boti yao alasiri na siyo ile
ya asubuhi na Simba.
“Hivi itawezekana
vipi mtu usafiri na adui wako? Kwetu hakuna kitu kama hicho wao kama
Simba wanaona sawa kusafiri na sisi kwenye boti sawa, lakini sisi kwetu
hapana hatuwezi,” alisema bosi huyo.
Alipotafutwa Meneja
wa Yanga, Hafidh Saleh kuzungumzia sakata hilo alisema: “Ni kweli
tulipanga tuondoke kesho (leo) saa moja asubuhi na boti la Kilimanjaro,
lakini tumebadili muda na tutaondoka saa tisa alasiri.”
Kwa upande wa Simba,
Mussa Mgosi alisema: “Sisi tunaondoka kesho (leo) asubuhi na tutaondoka
na kikosi chote tulichokisajili na nisingependa kuwazungumzia wapinzani
wetu.”Sign up here with your email