Polisi nchini
Ujerumani wana mtafuta kijana wa miaka 24, Anis Amri raia wa Tunia kwa
tuhuma za kuhusishwa na shambulio la lori katika soko la Christmas mjini
Berlin nchini Ujeruman,ambapo watu 20 waliuawa.
Anis ametajwa na
vyombo vya usalama nchini Ujeruman kuwa ni mmoja wa watu hatari na
anaye daiwa kujihusisha na mtandao wa makundi ya wapiganaji wa
Kiislam,ambapo idara za usalama zilianza kumtilia shaka kuwa anahusiana
na mtandao huo wa kigaidi tangu mwaka jana alipoingia nchini UjerumanDola laki moja zimetolewa kama zawadi kwa mtu yeyote atakayefanikiwa kukamatwa kwa Anis Amri,ambaye pia Polisi nchini humo wamebaini kuwa amekuwa akitumia majina sita tofauti huku akiwa na uraia wa nchi tatu tofauti.Julien Reichelt ni mhariri mwandamizi wa mtandao wa Bild,ameambia BBC kuwa tukio hilo bado haliingii akilini mwa waliowengi nchini humo.
Msemaji wa Polisi mjini Berlin wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanamkamata mshukiwa wa shambulio hilo amesema pia kuwa kutakuwa na mapitio ya hatua za kiusalama.
Maofisa usalama nchini Ujerumani wamesema kuwa Anis Amri alikuwa anaratajiwa kuondolewa nchini humo baada ya maombi yake ya hifandi kutokana na utata wa vielelezo vyake,ikiwemo pia hatua ya Tunia kumkataa kuwa hakuwa raia wa taifa lao.
Sign up here with your email