Tume ya Utumishi wa Umma imetaja mamlaka sita zenye dhamana na madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma kisheria ikiwa pamoja na kufuta nafasi za madaraka.
Vilevile,
Tume hiyo imezitaka mamlaka za nidhamu zote kuzingatia sheria, kanuni
pamoja na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya
hivyo, watumishi wanaotuhumiwa kufanya kosa watatendewa haki.
Tume
ya Utumishi wa Umma imetoa maelekezo hayo siku chache baada ya viongozi
wengi katika Serikali ya Awamu ya Tano wakiwamo wakuu wa mikoa na
wilaya kuwachukulia kiholela hatua za nidhamu watumishi wa umma wakati
baadhi hawana mamlaka hayo kisheria.
Baadhi
ya wakuu wa mikoa wamekuwa waki- wasimamisha watumishi hadharani tena
kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja bila kuwapa walalamikiwa
nafasi ya kujitetea, na wakati mwingine kudhalilishwa katika mikutano.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi Tume hiyo, Enos Mtuso
alisema kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 na
kanuni zake za mwaka 2003 madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu
watumishi wa umma yako chini ya watu wachache.
“Sheria
ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 ilitungwa ili kuweka misingi ya
kisheria katika kutekeleza malengo ya Sera ya Menejimenti na Ajira
katika Utumishi wa Umma iliyopitishwa na Serikali mwaka 1998.
Sheria
hii ndiyo inayotoa uwezo kwa mamlaka za kinidhamu mbalimbali katika
utumishi wa umma na kuweka misingi ya namna masuala hayo yanavyopaswa
kushughuliwa,” alisema.
Mtuso
alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Katibu Mkuu Kiongozi,
watendaji wakuu, wakuu wa idara na divisheni, na mamlaka za Serikali za
Mitaa (Baraza la Madiwani).
Lakini
alipoulizwa mkuu wa mkoa anapata wapi mamlaka ya kuwafukuza kazi
watumishi wa umma na kuwadhalilisha mbele ya hadhara, Mtuso alisema wao
kama Tume hawana mamlaka ya kuzungumzia jambo hilo kwani kwa kufanya
hivyo watakuwa wanakiuka maadili na kwamba suala hilo liko chini ya
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Kauli
ya Tume iliwekewa uzito na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Tamisemi), Seleman Jaffo ambaye amewataka wakuu wa idara kuacha
kuwanyanyasa wafanyakazi kwani hali hiyo inasababisha wafanye kazi kwa
hofu ya kutumbuliwa.
Akizungumza
baada ya kuwatembelea watumishi wa umma wa Manispaa ya Ilala, jijini
Dar es Salaam jana, Jaffo alisema wizara yake itatoa ushirikiano kwa
watumishi wote wanaofanya kazi kwa bidii.
Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.
Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.
Alisema
Watumishi hao wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo, kukiuka
maadili ya kazi, kutotekeleza majukumu, ubadhilifu, rushwa, wizi wa
fedha na mali, udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe, utovu
wa nidhamu huku utoro kazini ukiwa na idadi kubwa ya waliofukuzwa kazi.
“Utoro
kazini ni changamoto kubwa inayotukabili na ndiyo mashauri yake mengi
yanathibitika, unakuta mtumishi haendi kazini siku tano na kuendelea
bila sababu maalumu wala hatoi taarifa yoyote kwa waajiri wake kuwa
anashida gani,” alieleza.
Sign up here with your email