Tume
iliyoundwa na Mufti wa Tanzania , Sheikh Abubakar Zubeir mapema leo
Novemba 24 imekabidhi “Ripoti ya Tume ya Mufti” ya Mali za BAKWATA kwa
mkoa wa Dar es Salaam mbele ya wanahabari na kueleza kuwa mambo yote
wameyaorodhesha humo na baada ya kuipitia Mufti mwenyewe ndiye mwenye
mamlaka ya kuweka wazi.
Akipokea
Ripoti hiyo, Mufti amebainisha kuwa, kazi iliyofanywa ni nusu ya kazi
yenyewe iliyotarajiwa kuipata na kwa unyeti wa jambo hilo ameamua
kuwaongezea muda wa siku 90, yaani miezi mitatu ili waweze kuzunguka
nchi nzima.
“Nashukuru
kwa kazi muliyofanya. Kwa unyeti wa jambo lenyewe nimeamua kuwaongezea
muda kwani BAKWATA ipo karibu nchi nzima na nawongezea miezi mitatu. Kwa
kuwa sijui kipo ndani ya ripoti hii mpaka noisome, nadhani baada ya
hapo nikisha ipitia nitayafanyia kazi” ameeleza Mufti , Sheikh Zubeir.
Tume
hiyo yenye jopo la Wajumbe Nane akiwemo Mwenyekiti wa Tume hiyo
Sheikh Abubakar Khalid na akisaidiwa na Kaimu Mwenyekiti wa tume Sheikh
Issa Othuman Issa na wajumbe wengine sita akiwemo Katibu wa tume,
Mwalimu Salim Ahmed Abeid na wengine wanne.
MO tv:
Sheikh
Abubakar Khalid akimkabidhi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
ripoti ya Tume ya Mufti iliyochunguza Mali za BAKWATA kwa mkoa wa Dar
es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa tume hiyo, Sheikh Issa Othuman
Issa.
Sheikh
Abubakar Khalid akimkabidhi Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
ripoti ya Tume hiyo.Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa tume hiyo, Sheikh
Issa Othuman Issa.
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir
Kaimu
Mwenyekiti wa tume ya Mufti, Sheikh Issa Othuman Issa akielezea namna
Tume ilivyofanya kazi yake na kukabidhi ripoti hiyo mapema leo
Mwenuyekiti wa Tume ya Mufti, Sheikh Abubakar Khalid
Baadhi ya wajumbe wa tume hiyo
Ripoti ya tume hiyo
Makabidhiano ya ripoti hiyo
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir (katikati) akiwa pamoja na jopo la tume hiyo muda mfupi baada ya kukabidhiwa ripoti.
Sign up here with your email