MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya
utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma
zilizoandaliwa na Bodi ya
Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka 2015.
Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya
Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha
yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na
Wahasibu (NBAA).
“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika
nafasi ya kwanza kutokana na kuwasilisha
vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya
uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi
ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Bi. Mndeme.
Aidha Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu
kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa
mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA
inafanya kazi kwa ueledi na uwazi kupelekea
kupata tuzo ya heshima.
Katika mashindano hayo Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC) wameibuka washindi wa pili huku kampuni inayotengeneza Sementi (Tanga Cement Plc) wakiibuka kuwa washindi wa
jumla kwenye tuzo hizo .
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna
Mndeme kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za
umma kutoka kwa Mwakilishi wa Mhasibu
Mkuu wa Serikali Bw .Shogolo
Msangi katikati wakati wa sherehe za
kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji
bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
wa kwana kushoto ni Mwenyekiti wa NBAA Prof. Isaya Jairo.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
Dkt.Ayoub Rioba kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za
umma baada kuwa mshindi wa pili kutoka
kwa kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali
Bw .Shogolo Msangi kushoto wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika
nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Afisa Mkuu wa Mapato kutoka kampuni ya kutengeneza
sementi (Tanga Cement Plc) Bw. Pieter De Jager wa pili kulia akiwa ameshika
tuzo ya washindi wa jumla kwenye masindano ya wawasilishaji bora wa mapato kwa
mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw .Shogolo Msangi katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na
washindi wa uwasilishaji bora wa mapato wakati
wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya
jiji la Dar es salaam.
Sign up here with your email