TANESCO YATANGAZA KUWEPO KWA KATIZO LA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA - Rhevan Media

TANESCO YATANGAZA KUWEPO KWA KATIZO LA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA


umeme
 Mhandisi wa umeme wa Shirika la Umeme nchuini Tanzania TANESCO, akiwa kazini jijini Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme
Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida,
Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara,
Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya
Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na
Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City,
Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya
Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.


SABABU: Kuruhusu
Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya
Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa
hadi Shinyanga.

SABABU: Kuzimwa
kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam
ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.


Matengenezo hayo
yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.
  
Uongozi unaomba
radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na;
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao
Makuu


Previous
Next Post »