Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo David Mziray MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
……………………………………………………………………………………
Na Lilian Lundo-MAELEZO-Dar es Salaam
MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri
wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imeunda kikosi kazi maalum kwa ajili ya
kudhibiti upandashaji holela wa nauli kwa mabasi yaendayo mikoani
wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Hayo yamesemwa leo na Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka hiyo David Mziray wakati wa mahojiano na
mwandishi wa habari hii, akieleza namna mamlaka hiyo inavyodhibiti
upandaji wa nauli za mabasi yaendayo mikoani.
“Kuna timu ambazo ziko katika
vituo vyote vya mabasi makubwa katika kila mkoa, timu hizo zinathibiti
masuala ya nauli, usalama wa magari , kuhakikisha leseni za mabasi
pamoja na muda uliopangiwa kuondoka vituoni,” alifafanua Mziray.
Aliongeza kuwa mamlaka hiyo
imeruhusu mabasi yanayobeba abiria 40 na kuendelea kuomba leseni za
muda za kusafirisha abiria katika mikoa ambayo ina wasafiri wengi zaidi
katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Kwa mujibu wa Mziray alisema
mabasi hayo yatakuwa yakikaguliwa kwanza ndipo yanapewa leseni za muda
pamoja na kupangiwa nauli ambazo watatozwa abiria kutokana na mkoa ambao
gari hilo litakwenda.
Akizungumzia kikosi kazi hicho,
Mziray alisema kuwa mwanzoni mwa wiki hii timu iliyoko kituo cha mabasi
cha Ubungo ilikamata mabasi manne ambayo yalipandisha nauli kwa abiria
na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Sign up here with your email