Shirika la
kibinaadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vikosi vya usalama ini
DR Congo vimewaua takriban watu 34 wakati wa maandamano wiki hii.
Mazungumzo
yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili
kujaribu kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila
ambaye alikataa kuondoka madarakani wakati muda wake ulipokamilika siku
ya Jumatatu.Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine 17 wameuawa kaskazini magharibi mwa Congo.
Hali ya utulivu yerejea nchini DR Congo
Watu 20 wauawa katika maandamano DR Congo
Baraza jipya la mawaziri latangazwa DR Congo
Maafisa wa polisi wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu linaloamini kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa dunia.
Wakati huohuo Mamlaka nchini DRCongo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Lubumbashi.
Meya wa mji huo anasema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu, japo wenyeji wa mji huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.
Sign up here with your email