Trump amesema hayo ni matukio ambayo alikuwa anategemea yatatokea ndiyo maana wakati wa kampeni zake akaweka wazi kabisa kuwa anataka kuona watu wenye imani za Kiislamu wanazuiliwa kuingia Marekani kwani ndiyo wanahusika na mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mengi duniani.
“Jambo linaloendelea sasa nila kutisha, linatisha, mpango wangu kwa haya yanayotokea sasa nimethibitisha kuwa nipo sahihi kwa asilimia 100. Kinachotokea sasa ni aibu,” alisema Trump.
Trump alisema ni vyema Waislamu wakazuiliwa kuingia Marekani kwani wanaweza kufanya vitendo vya kigaidi ambavyo vitaifanya Marekani kupoteza amani iliyopo sasa na kuifanya kuwa nchi ya magaidi.
“Matukio haya niya uonevu, lazima yazuiliwe,” alisema Trump ambaye hivi karibuni anataraji kuchukua kiti cha Urais wa Marekani ambacho kwa sasa kinakaliwa na Barack Obama.
Sign up here with your email