SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI (JWTZ) KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAANZA - Rhevan Media

SAFARI YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI (JWTZ) KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAANZA


Waandishi wa Habari walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakinyanyua mikono kuashiria kuanza safari hiyo katika lango la Marangu.
Safari ya kupanda ikaanza katika lango la Marangu majira ya saa 5 asubuhi kila mmoja akiwa na nguvu za kutosha na shauku ya kutizama mandhari ya Mlima Kilimanjaro ambao siku ya kwanza safari inaanza kwa kupita katika msitu mnene.
Wapandaji waliokuwa wamevalia nguo za kuzuia baridi mapema wakati safari ya kupanda mlima inaanza baadae kidogo kidogo walilazimika kuzipunguza kwa sababu pindi unapotembea joto la mwili pia huongezeka.
Safari ya kupanda mlima kwa kundi hili la Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,George Waitara lilikuwa pia na ulinzi wa kutosha.  



Previous
Next Post »