MKUU wa mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Stevene Kebwe amesema mkoa huo kwa sasa una ziada ya chakula cha tani Milioni 1 na laki 3 katika akiba iliyotokana na uzalishaji wa mwaka 2015/2016.
Kebwe amesema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa globu ya jamii juu ya mafanikio ya uzalishaji wa chakula katika mkoa huo, ambao una sifa ya kuwa na udongo wenye rutuba na hali ya hewa nzuri.
“Katika kipindi cha uzalishaji cha mwaka 2015/2016 tumefanikiwa kuzalisha jumla ya tani milioni 1 na laki 8 na huku mahitaji yakiwa ni tani laki tano katika mkoa wetu,hivyo uzalishaji huo umetufanya tuwe na zida kubwa ya kufikia Milioni 1 na laki 3 tukiwa tunafunga mwaka wa 2016’’amesema Kebwe.
Ameongeza kuwa katika mwaka huu uzalishaji wa mazao ya shabni uko vizuri, hali inayoashiria hakutakuwa na njaa katika mkoa huo na badala yake ziada ya chakula kinachopatikana hapa kitaweza kulisha mikoa ya jirani.
Ametaja kuwa licha ya kuwa na mafanikio makubwa katika kilimo cha mashambani,bado kumekuwa na changamoto kubwa ya ongezeko la mifugo katika mkoa huo kulinganisha na eneo ambalo lililopo na mahitaji yanayohitajika kutokana na hesabu za kitaalamu.
Amesema kuwa serikali yake ya mkoa imejipanga kuhakikisha kuwa inatoa elimu kwa wafugaji kupunguza mifugo mingi na kuwa na mifugo yenye tija ambayo italeta faida kiuchumi kwa muda mfupi hili kupunguza migogoro ya malisho baina ya wakulima na wafugaji.
Sign up here with your email