Bingwa wa zamani wa
mchezo wa Tennis Wimbledon, Petra Kvitova, amefanyiwa upasuaji kwenye
mkono wake kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa
kisu katika moja ya miji ya Jamhuri ya Chekslovakia.
Akiandika
kwenye ukurasa wake wa kijamii , ameeleza kuwa alishtushwa na
shambulizi hilo na anajiona ana bahati kuwa hai baada ya kujitetea
mwenyewe dhidi ya shambulizi hilo.Msemaji wa bingwa huyo wa zamani ambaye anapewa nafasi ya kumi na moja kwa ubora duniani kwenye mchezo wa tenisi, amesema kwamba, afya ya bingwa huyo itatengamaa baada ya miezi mitatu.
Petra Kvitova aliwahi kuwa bingwa mchezo wa tenisi wa Wimbledon mwaka wa 2011 na 2014.
Sign up here with your email