MRADI MKUBWA WA UMEME WA BACKBONE UMEKAMILIKA, KUZINDUALIWA JANUARI - Rhevan Media

MRADI MKUBWA WA UMEME WA BACKBONE UMEKAMILIKA, KUZINDUALIWA JANUARI

 Meneja wa mradi mkubwa wa umeme wa Backbone, Mhandisi Khalid Reuben James, akitoa maelezo kwa wahariri (jawapo pichani), walipotebelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Tagamenda kilichoko nje kidogo ya mji wa Iringa, wakati wa ziara ya wahariri kukagua ujenzi wa mradi wa Backbone unaotoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma na Singida, Desemba 19, 2016

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;}


MRADI
wa umeme wa Backbone wa ujenzi wa njia kuu ya umeme ya msongo wa Kilovolti 400
ya urefu wa Kilomita 670 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Dodoma
na Singida, umekamilika kwa asilimia 100, Meneja wa Mradi huo, Mhandisi
Khalid Reuben James amewaambia wahariri wa vyombo vya habari mjini Iringa leo
Desemba 19, 2016.
Pia
mradi huo unaohusisha kukamilika kwa
upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme kwenye mikoa ya Iringa,
Dodoma, Singida na Shinyanga utawezesha kuvipatia umeme vijiji takriban 121, vinavyopitiwa
na mradi huo, alisema Mhandisi James.
“Mradi
huu ni wa muhimu sana kwenye gridi ya taifa kwa sababu utaongeza uwezo wa
kusafirisha umeme kutoka kanda ya Kusini Magharibi, ambako kuna vyanzo vingi
vya umeme na kupeleka Kanda ya Kaskazini Magharibi ambako kuna shughuli nyingi
za kiuchumi ikiwemo migodi ya madini.” Alifafanua Mhandisi James.
Kwa
mujibu wa Mhandisi huyo, mradi huo ulianza mwaka 2013, na ulikadiriwa kugharimu
kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 470, ambazo zimetolewa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wafadhili wakiwemo, Benki ya Dunia, dola za
Kimarekani, milioni 150, Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB),  na Shirika la Maendeleo la Kijapani, (JICA),
Dola za Kimarekani milioni 129.7, Benki ya Uwekezaji ya nchi za Jumuiya ya
Ulaya, (EIB), Dola za Kimarekani milioni, 134.5, Shirika la Kiuchumi la
Maendeleo ya Korea ya Kusini, (EDCF), Dola za Kimarekani milioni 36.416, na
Serikali ya Norway, Sweden na Tanzania, kupitia kwa wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Dola za Kimarekani milioni 33.4.

Ndugu zangu, mradi huu unatoa hakikisho kwa serikali kuwa mipango yake ya
kujenga uchumi wa viwanda unawekana pasina shaka, kwani mradi huo mkubwa, utawezesha
sasa, kuwapatia wateja umeme ulio bora na wa uhakika,” alsiema.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wako kwenye ziara ya
kutembelea mradi huo ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mapema mwezi Januari,
2017.
 Wahariri wakitembelea mitambo ya umeme kituo cha Tagamenda
 Mhandisi huyu wa Tanesco, akitumia ramani ya mradi huo kuwaelimisha wahariri ukubwa wa mradi huo
 Wahariri wakiangalia nguzo zinazobeba nyaya (conductors), za mradi wa Backbone, kwenye kituo cha Tagamenda
 Mhariri wa Business Times, Imma Mbuguni, akipita kwenye moja ya mnara mkubwa wa kupitisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kwenye bwawa la Mtera, mpakani mwa mikoa ya Iringa na Dodoma Desemba 19, 2016



 Hii ni moja ya nyumba za askari polisi kituo cha polisi mtera, ambayo TANESCO walilipa mfidia kwa mmiliki wa nyumba hiyo ili kupisha mradi na kumjengea nyumba nyingine mita inayoonekana kipande kushoto
 Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kama fidia kwa mmiliki wa nyumba ya awali aliyepisha mradi huo
 Bwawa la kufua umeme la Mtera lililoko mpakani mwa mikoa ya Iringa na Dodoma
 Wahariri wakipatiamaelezo ya kiufundi kuhusiana na mradi huo kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Taganenda
 Wahariri wakitembelea chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme kwenye kituo cha Taganenda mkoani Iringa
 Mhandisi James, akiongozana na baadhi ya wahariri na maafisa uhuisno wa TANESCO baada ya kutembelea bwawa la kufua umeme la Mtera
 


 Mhandisi James, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa Backbone
 Mhandisi James, (aliyevaa kkikoti akisi), akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wa Backbone

Previous
Next Post »