MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANA PAROKIA WENZAKE KUSALI IBADA YA JUMAPILI - Rhevan Media

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANA PAROKIA WENZAKE KUSALI IBADA YA JUMAPILI


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.

Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema. "Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.

"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.

"Kwa kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia, tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu" ameongeza Epifania Ngonyani.

Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea komuniyo kutoka kwa Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 
1Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. wa kwanza kulia kwake ni Dada yake Ester Enock na anayefuata ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa. 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.


Previous
Next Post »