Jeshi la polisi limesema limeimarisha ulinzi kuelekea sikukuu za Kristimasi na mwaka mpya hili kudhibiti vitendo vya uharifu .
Akizungunza leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema jeshi la polisi katika kipindi cha sikukuu kuna watu wanajipanga kufanya uhalifu hivyo jeshi la polisi litafanya doria za kutosha.
Amesema kumbi zote zinazofanya starehe za kupiga mziki ziingize watu kutokana na ukumbi na watakaozidisha watachukuliwa hatua.
Afande Advera amesema wataondesha vyombo vya moto wataobainika wametumia vilevi watachukuliwa kwani nia yao nikutaka kusababisha ajali.
Aidha amesema wazazi wanatakiwa kufanya ulinzi kwa watoto wao kutokana na watoto kupotea katika siku za sikuu na kusababisha vituo vya polisi kuwepo kwa watoto hao.
Hata hivyo amesema wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapohisi kuna watu wanaashiria kufanya uhalifu.
Advera amesema kuwa wale ambao watatoa taarifa zikashindwa kutekelezeka wawasiliane na ngazi ya juu ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watu waliofanya uzembe.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba
Sign up here with your email