Kwenye mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi, Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na wachezaji wote wakiwa na ari kubwa licha ya kuwepo kwa taarifa za majeraha kwa mlinzi Haruna Shamte aliyeumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Kama unavyofahamu jumamosi iliyopita tulipata suluhu ya 0-0 na Kagera Sugar, mara hii tunafanya maandalizi makubwa kuhakiksha tunashinda mchezo ujao, pointi tatu ni jambo pekee linalohitajika kwenye duru hii ya pili, tunaifahamu Toto kuwa ni timu nzuri lakini mara kadhaa sisi tumekuwa tunaibuka wababe dhidi yao, alisema
Akiendelea zaidi Ten aliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo dhidi ya Toto, City inaweza kukosa huduma ya mlinzi wake Haruna Shamte aliyepata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo uliopita ingawa jopo la madaktari wameahidi kutoa taarifa mpya juu yake siku ya kesho huku akigusia pia suala la ITC ya kiungo Mrisho Ngassa.
Shamte alipata majeraha kwenye mchezo uliopita, huenda asiwepo kikosini jumamosi, ingawa hili litategemea na ripoti ya daktari siku ya kesho, kuhusu Mrisho Ngassa ni kweli ITC yake ilichelewa, hii ni kwa sababu ijumaa na jumamosi ni siku ya mapumziko huko Oman, tulizungumza nao jana wakaahidi kututumia leo, hivyo tuna uhakika leo wataituma na ni wazi atakuwa sehemu ya kikosi kwenye mchezo huo,alimaliza.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha City wakipata maji ya kunywa kwenye mazoezi leo asubuhi
Sign up here with your email