Mji wa Auckland nchini New Zealnd ndio mji wa kwanza duniani kuukaribisha mwaka mpya wa 2017.
Fataki zilirushwa kutoka jengo refu katikati mwa mji huo.Polynesia na visiwa vya Pacific ikiwemo Samoa, Tonga na kiribati pia viliukaribisha mwaka mpya.
Miji mingi duniani imeimarisha usalama kwa sherehe za mkesha wa mwaka mpya baada ya mwaka ambapo washambuliaji waliendesha malori katika umati wa watu mjini Berlin na Nice.
Mjini Paris Madrid na New York vizuizi vya simiti na magari yaliobeba mizigo mizito yatatumiwa kuzuiwa bustani zilizopo mjini ambapo watu wengi hukongamana ili kusherehekea.
Sign up here with your email