CHINA YAKUBALI KUIREJESHA MANUWARI YA MAREKANI - Rhevan Media

CHINA YAKUBALI KUIREJESHA MANUWARI YA MAREKANI

Manuwari ya Marekani iliokamatwa na China

 Manuwari ya Marekani iliokamatwa na China
Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon imesema kuwa imeafikiana na China kwamba itairejesha manuwari iliopatikana katika bahari ya kusini mwa China.
China iliikamata manuwari hiyo katika maji ya kimataifa siku ya Alhamisi.
Haijasema ni kwa nini ilichukua hatua hiyo na kuishutumu Marekani kwa kulifanya jambo hilo kuwa kubwa.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameishutumu China kwa kuiiba meli hiyo ,huku akisema: Tunafaa kuiambia China kusalia na manuwari hiyo walioiba, aliandika katika mtandao wake Twitter.
Kisa hicho ni miongoni mwa visa vibaya zaidi vya makabiliano ya kijeshi kati ya mataifa hayo yenye uwezo mkubwa wa kijeshi katika kipindi cha miongo kadhaa.
Trump aitaka China kuhifadhi manuwari ya Marekani
Pentagon imesema kuwa manuwari hiyo inayojulikana kama UUV ilikuwa ikitumika kubeba utafiti wa kisayansi wakati ilipokamatwa na kutaka irejeshwe mara moja.
Imeionya China kutochukua hatua kama hiyo katika siku zijazo.
Lakini msemaji alisema siku ya Jumamosi kwamba mataifa hayo mawili yameafikiana.
''Kupitia mazungumzo na mamlaka ya China,tumeafikiana kwamba China itarejesha chombo hicho kwa Marekani '',alisema msemaji wa Pentagon Peter Cook katika taarifa.
Wizara ya ulinzi nchini China imesema kuwa meli hiyo itarudishwa katika njia ilio sawa.
Haijulikani ni lini hatua hiyo itatekelezwa.
Previous
Next Post »