Israel
imewatahadharisha raia wake dhidi ya safari za kwenda India wakisema
kuna hatari kubwa huenda wakashambuliwa wakiwa huko.
Wameonya
hasa waepuke maeneo ya vivutio vya watalii vilivyoko kusini mashariki
mwa nchi hiyo, ikiwemo maeneo ya fuo za bahari na hata vilabu vya
burudani za usiku kama disco wakisema huenda kukawa na mashambulio
wakati wa mkesha wa mwaka mpya. Mwandishi wa BBC huko Jerusalem anasema Israel hutoa tahadhari kama hizo mara kwa mara lakini ni nadra kwamba wanataja maeneo maalum kama hayo.
Sign up here with your email