“Sielewe ni nini” ni kauli ya Dk. Mpango mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam alipozungumzia hali ya uchumi kuanzia Julai mpaka Disemba mwaka huu na matarajio ya mwaka 2017.Kuyumba kwa biashara kumesababisha zaidi ya maduka 1,800 kufungwa ndani ya miezi mitatu.
Amethibitisha kwamba, mapato yaliyokuwa yakipatikana kutokana na biashara ya maduka ya jumla na rejareja yamepungua kutokana na maduka hayo kufungwa yakiwemo 1,872 baada ya kuyumba kibiashara.
Wilaya zenye maduka hayo zilizoathirika kutokana na kuyumba kwa biashara jijini Dar es Salaam ni pamoja na Kinondoni ambapo maduka 443 yamefungwa, Temeke (222), Ilala (1,076) na Arusha 131.
Kwa kauli ya Dk. Mpingo, miongoni mwa maduka yaliyofungwa ni yale yaliyokuwa yakifanya biasahra za jumla na rejareja, yanayojihusisha na vyombo vya usafiri pamoja na vifaa vya ujenzi.
Amesema kuwa, mpaka sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika ili kubaini sababu za maduka hayo kufungwa na kwamba, hisia zinazotawala ni kuwepo kwa changamoto katika kuyaendesha.
“Sababu hasa za biashara hizo kufungwa hazijabainika kutokana na ugumu wa kupata taarifa hizo kutoka kwa wenye biashara zilizofungwa,” anasema.
Sign up here with your email