YALIYOJIRI ZIARA YA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM. - Rhevan Media

YALIYOJIRI ZIARA YA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM.


15
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Vijana walioathirika na madawa ya kulevya (hawapo pichani) alipotembelea kituo cha Sober House cha kurekebisha waathirika wa dawa za kulevya kilichopo Vijibweni Kigamboni wakati wa ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwaajili yakusikilza kero za wananchi.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
2
Kulia ni Kijana mmoja aliyeko kwenye kituo Sober House cha kurekebisha waathirika wa dawa za kulevya, kilichpo Vujibweni Kigamboni, akimuonyesha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda tumbo lake lilivyobaki na makovu ya kutisha kutokana na operesheni aliyofanyiwa kutolewa dawa za kulenya tumboni
3
Baadhi ya Vijana walioathirika na madawa ya kulevyo wakipiga makofi kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akizungumza.
14
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akipokea zawadi kutoka kwa  Mmiliki wa Kituo cha  vijana wa Sober House,Nuru Saleh leo jijini Dar es Salaam.
4
Wageni waalikwa mbalimbali.
Mbunge wa Kigamboni  Dk, Ndugulile akiwa na DAS wa wilaya ya Kigamboni Lahel Mhando wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
5
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
6
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijibu kero za  wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kigamboni na kusikiliza kero mbalimbali.
Ambapo amehaidi kuwasiliana na viongozi wa usalama wa Taifa ili kuwaombea jengo lililoacha na hayati Aboud Jumbe ili walitumie kama ofisi, pia amepiga marufuku uchimbaji wa kokoto kwa eneo la Mji Mwema kwani unachochea uharibifu wa Mazingira,hatarishi kwa usalama wa wakazi waishio maeneo , pia maeneo hayo yanaweza kutumika kwa vitendo vya uhalifu.
7
Mbunge we jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndugulile akielezea changamoto wanazozipata wananchi wa Kigamboni.
8
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro akizungumza.
9 10 11 12 13
Wananchi mbalimbali wakimuelezea Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kero wanazozipata.
Previous
Next Post »