Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba amewataka vijana wasisite kuleta mabadiliko chanya katika Nchi
mana Vijana ndiyo tegemeo la Taifa.
Ameyasema
hayo mjini Unguja alipokua akizindua Baraza la Vijana la Wilaya ya
Magharibi A mjini Kisiwani Zanziba. Amewasishi Vijana watumie baraza
hilo kama tanuri ya kutengenezea mbinu za uongozi na pia kama daraja la
kuanzishia vikundi vya ujasiriamali na uzalshaji mali na kutengeneza
njia mbalimbali za kuinua uchumi na kutowafanya kuwa tegemezi.
Akijibu
risala ya Vijana hao ambayo imesomwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo la
Vijana Bi Farida Juma ambapo walitaja changamoto zinazowakabili ni
pamoja na uhaba wa fedha, Waziri Makamba amelitaka Baraza hilo kufungua
akaunti na yeye atawapatia mchango wake wa shilingi milioni mbili.
Awali
akimkaribisha Mheshimwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A,
Mheshimiwa Mwinyiusi Hassan amewataka vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa na
pia wahakikishe wanalinda na kuheshimu na kuulinda utamaduni wa Nchi
yetu.
Wakitoa
shukrani zao kwa Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Baraza hilo la Vijana
walimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuitikia wito wao wa kumuomba awe
mgeni Rasmi katika siku yao hiyo adhimu.
Waziri
Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akihutubia wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Wilaya ya
Magharibi ‘A’ mjini kisiwani Zanzibar ambapo alkua Mgeni Rasmi.
Waziri
Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Magaharibi A Mh. Mwinyiusi
Hassan wakati aliposhiriki uzinduzi wa baraza la vijana la wilaya hiyo
kama Mgeni Rasmi.
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri
Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza hilo .
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri
Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akionyesha cheti kama ishara ya uzinduzi wa Baraza la Vijana
wilaya ya Magharibi A.
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri
Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Magharibi A, Mh
Saada Mkuya, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Bi. Farida Juma na Mkuu wa
Wilaya ya Magaharibi ‘A” Mh Mwinyiusi Hassan.
Mgeni
Rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Vijana Wialaya Magharibi A, Waziri
Wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January
Makamba akifurahia zawadi alizopatiwa na Braza la Vijana Wilaya ya
Magharibi A.
Sign up here with your email