Imeelezwa kuwa Juhudi za serikali katika kutafuta suruhisho ya migogoro ya wakulima na wafugaji inaweza kufanikiwa endapo serikali itatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya wafugaji zikiwemo za ujenzi wa miundo mbinu na usimamiaji wa sheria ya matumizi bora ya ardhi.
Wakiongea katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabili wafugaji mkoani morogoro wamebainisha changamoto zinazo wakabili hadi kupelekea ugumu wa shughuli zao za kila siku ni pamoja na ufinyu wa maeneo waliyonayo ,maji ya kunyweshea mifugo na ukosefu wa miundo mbinu kama shule na zahanati huku swala la upigaji chapa wakidai halijaonesha umuhimu uliopo kwao licha ya kuwa baadhi yao waliitikia kutekeleza zoezi hilo.
Kwa upande wake mtafiti masuala ya wafugaji,mkoa wa morogoro adam ole mwarabu amesema miongoni mwa watu wanaosabisha migogoro ni madalali na baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanauza ardhi kinyume na utaratibu na kusababisha migogoro ambapo ameiomba tume ya taifa ya matumizi ya ardhi itunge sheria na kusimamia ili kukombesha viongozi wenye tabia hizo.
Sign up here with your email