WAFANYABIASHARA MWANZA HAWATUMII EFD - Rhevan Media

WAFANYABIASHARA MWANZA HAWATUMII EFD

Tokeo la picha la EFD machineBAADHI ya wafanyabiashara wa   Mwanza wanaendelea kufanya biashara zao kwa kuuza bila ya kutoa Stakabadhi za Mashine za Elektroniki (EFD).
Wafanyabiashara hao wanadai  wanangoja Serikali ianze kuwasambazia mashine hizo.
Kwa sababu hiyo wamekuwa  wakitoa  stakabadhi za kawaida hali ambayo inaelezwa kuwa huenda imekuwa ikiikosesha mapato Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na MTANZANIA kwa sharti la kutotaja majina yao, walidai  Serikali iliahidi kuzigawa mashine hizo bure  kwa wafanyabiashara   waweze kuzitumia kulipa kodi pale mteja anaponunua bidhaa zao lakini hadi sasa hazifikishwa.
Walisema baada ya ahadi ya Serikali kutolewa, mashine hizo zilitolewa kwa wafanyabiashara wa Dar  es Salaam lakini mpaka sasa hawajui ni lini zitafikishwa na kusambazwa mkoani  Mwanza.
Wafanyabiashara hao wameiomba Serikali kutekeleza ahadi yake ya kuzigawa mashine hizo.
Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee,   alisema suala hilo liko juu ya uwezo wake kwa sababu anayetakiwa kuelezea mashine hizo ni kamishna mkuu wa mamlaka hiyo.
“Ninachojua wapo baadhi ya wafanyabiashara wanazo mashine hizo za EFD na wanazitumia lakini wale ambao hawana wanatakiwa kutekeleza sheria za ulipwaji wa kodi na wanapaswa kutoa stakabadhi.
“Suala la mashine kusambazwa   bure mimi siwezi kulizungumzia ni vema mkamuuliza kamishna mkuu kule Dar es Salaam.
“Lile ni tamko la taifa, sasa utekelezaji wa tamko hilo unaamuliwa huko huko, mimi hapa sina uamuzi wowote,” alisema.
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa wanachama wa  Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) ambao  wamekuwa katika mgogoro w amuda mrefu  na TRA juu ya matumizi ya stakabidhi ya EFD na kusababisha maduka kufungwa.
Wafanyabiashara hao   chini ya Mwenyekiti wao wa  JWT, mkoa wa Mwanza, Christopher Wambura  wamekuwa na msimamo mkali  juu ya suala hilo.
Kitendo cha kufungwa maduka husababisha TRA kushirikiana na polisi kuwaonya  wale wanaohamasisha   au kuwatisia  wafanyabiashara walio na EFD kutotumia  mashine hizo.
Previous
Next Post »