TSHABALAL ATULIZA PRESHA ZA MASHABIKI SIMBA,AONGEZA MKATABA MPYA - Rhevan Media

TSHABALAL ATULIZA PRESHA ZA MASHABIKI SIMBA,AONGEZA MKATABA MPYA


zimbwe-3

Hatimaye uongozi wa Simba umewashusha presha mashabiki wake baada ya kumsainisha tena beki wake Mohamed Hussein Zimbwe kutokana na kuonesha umahiri katika kikosi cha kocha Joseph Omog.

Zimbwe maarufu kama Tshabalala amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya makubaliano yaliyofanyika wiki moja na nusu iliyopita.

Simba ilikubaliana na Zimbwe mbele ya baba yake mzazi na meneja wake, Herry Mzozo na leo ametia saini mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.

Tshabalala ambaye alishindwa kuaminiwa na Azam FC alifanya vizuri akiwa na Kagera Sugar kabla ya kusajiliwa na Simba ambapo kazi yake imeendelea kuonekana ndani ya klabu hiyo kongwe kwenye soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Mkataba huo mpya kati ya Simba na Tshabalala sasa unakata kelele zote kuhusu nyota huyo kujiunga na klabu yoyote katika kipindi hiki cha miaka miwili bila kuvunja mkataba.

Previous
Next Post »