WAKAZI wa Wilaya ya Tarime kwa mara ya kwanza wameandamano kwa amani kupinga vitendo vya ukeketaji wakati wazee wa mila wakiwa wametangaza kuanza kwa msimu wa ukeketaji Desemba 15, mwaka huu.
Maandamano hayo yaliyofanyika jana, yalisimamiwa na kuratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) kwa ufadhili wa Shirika la Forward UK and Comic Relief UK.
Yalipitia a mitaa mbalimbali ya mji wa Tarime na kupokewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga.
Luoga, akipokea maandamano hayo, alisema wahusika wa ukeketaji huo watakamatwa na kfunguliwa mashtaka.
Alisema iwapo polisi watasimamia wajibu wao na kuanza kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua, ukeketaji utatokomezwa haraka na kubaki historia hivyo kukomesha kwa kiasi kikubwa kwa mila hiyo potofu.
Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Bomani, Amosi Mapuli alisema wanaendelea na utafiti na kuwabaini watu wanaochochea vitendo hivyo kuendelea kuwap.
Alisema watachukuliwa hatua ingawa baadhi yao wanatoka nje ya nchi.
“Jeshi la polisi kwa ushirikiano na wananchi tumebaini kuwa kuna baadhi ya watu kutoka Kenya wanachochea ukeketaji.
“Watu hao wanaleta watoto wao kuja kukeketa hapa Tanzania jambo ambalo tunalifanyia utafiti na ikibainika kuwa ni kweli hatua zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Mapuli.
Mkurugenzi wa shirika hilo, Coshuma Mtengeti, alisema lengo la maandamano ni baada ya kugundua kuwa bado ukeketaji unaendelea.
Alisema hata tarehe rasmi ya kuanza ukeketaji imetangazwa na wazee wa mila huku koo nyingine zimeanza kukeketa.
Sign up here with your email