STEVE RNB AWAPONZA MASHABIKI WAKE. - Rhevan Media

STEVE RNB AWAPONZA MASHABIKI WAKE.

Steve RnB adai hatokaa kimya tena kama ilivyokuwa mwanzo na sasa amekuja na wimbo uitwao ‘Twende Wote’.
14334781_1275006289185031_3761042890478845952_n
Muimbaji huyo amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu alipoachia wimbo wake ‘Listen’ mwezi Februari mwaka huu.
Akiongea na Bongo5, Steve amesema, “Nimekuwa kimya tangu nilipoachia wimbo wa ‘Listen’ mwanzoni mwa mwaka huu, changamoto kubwa ikiwa ni tour ndefu niliyokuwa naifanya na band yangu ya In Africa ila kuanzia sasa naahidi sitowaweka tena mashabiki wangu muda mrefu bila ya kuachia wimbo mpya niwepo nchini au hata nikiwa nje.”
Usikilize hapa chini wimbo huo mpya ‘Twende Wote’ wa msanii huyo uliotayarishwa kwenye studio za Sei Rec.
Previous
Next Post »