Serikali imezindua rasmi maabara ya kupima ugonjwa wa kifua kikuu TB kwa kutumia Panya Buku ubunifu ambao umetekelezwa na chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine SUA kwa kushirikiana na taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya utafiti APOPO ya Ubelgiji ambapo sasa wagonjwa wa TB wataweza kupata majibu ya vipimo vya ugonjwa huo katika kipindi cha saa 24.
Maabara hiyo iliyopo katika maabara ya mifugo temeke vetenari itakuwa na uwezo wa kupima makohozi kwa kutumia Panya hao ambao wanagundua maambukizi ya ugonjwa huo kwa kunusa wana uwezo wa kutoa majibu ndani ya saa 24 ukilinganisha na vipimo vya maabara ambavyo wakati mwingine vinashindwa kubaini ugonjwa huo kumfanya mgonjwa kuendelea kushambuliwa na vijidudu vya ugonjwa huo hatua mabyo inachangia kusabibisaha kuenea kwa watu wengine.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara hiyo kwa niaba ya waziri wa Afya, mkurugenzi wa uhakiki ubora wa huduma za afya Mohamed Ally Mohamed amebainisha kuwa endapo panya hao wataweza kugundua wagonjwa wengi zaidi wakiwa katika hatua za awali hatua hiyo itasaidia pia katika kutoa fursa kwa waginjwa kupata matibabu kwa wakati na kuzuia maabukizi kwa watu wengine kwa kiasi kikubwa hivyo katika kufanikisha utafiti serikali itashirikiana na SUA na APOPO katika kuendeleza teknolojia hiyo.
Mkuu wa idara ya uwekezaji rasilimali watu idara ya maendeleo ya kimataifa DFID JANE MILLER ambao ndio wafadhili wa mradi huo kupitia mfuko wa maendeleo ya ubunifu rasilimali watu – HDIF amebainisha kuwa Tanzania inakabiliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo Kifua kikuu, HIV na malaria ambayo yamekuwa yakichukua nafasi ya juu ukilinganisha na magonjwa mengine hivyo uwepo wa maabara hiyo utapunguza maabukizi ya ugonjwa wa TB kwa kiasi kikubwa.
Sign up here with your email