RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HIFADHI ZA JAMII - Rhevan Media

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI HIFADHI ZA JAMII


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Joh Pombe Magufuli, leo amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi za hifadhi za jamii hapa nchini, za PSPF na LAPF.
Kwenye uteuzi huo Rais Magufuli amemteua Mhandisi Alhaji Mussa Ivombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), ambapo kabla ya uteuzi huo Alhaji Mussa Ivombe alikuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 
Pia Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Makamo Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi, Prof. Faustine Karani Bee kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF).
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Prof. Tadeo Andrew Satta kuwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, ambaye awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo. 
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, kupitia Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.
Previous
Next Post »