Cuba inaadhimisha
siku tisa za maombolezo kufuatia kufariki kwa Fidel Castro,
anayejulikana kwa siasa zake za kimapinduzi, aliyetawala taifa hilo kwa
miongo kadhaa na ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 90.
Mwili
wake, utachomwa hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe ya
kibinafsi, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu kote
nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Desemba
tarehe nne.Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani.
Donald Trump asema Fidel Castro alikuwa ‘dikteta katili’
Watu wengi katika mji mkuu wa Havana walidondokwa na machozi kwa kuwa kiongozi shujaa aliyeweza kukabiliana na Marekani katika uwanja wa kidiplomasia kwa miongo kadhaa, licha ya mbinu nyingi zilizofanywa za kutaka kumuua.
Kwa Picha: Maisha ya Fidel Castro
Waasi wa Serikali ya Castro hata hivyo walisherehekea kote duniani, walikotorokea.
Sign up here with your email