MAKINDA ASHANGAA UCHELEWESHWAJI SHERIA YA NDOA - Rhevan Media

MAKINDA ASHANGAA UCHELEWESHWAJI SHERIA YA NDOA

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda amesikitishwa kuona kuwa hadi leo serikali imeshindwa kufanyia marekebisho baadhi ya vifungu vilivyopo katika sheria ya ndoa.
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda.

Mhe. Makinda ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kwanza kitaifa la kutetea na kusimamia haki za wanawake kwa kuwawezesha kisheria na kiuchumi kongamano ambalo limefanyikia mkoani Dar es Salaam na kuudhuriwa na wanaharakati wa haki za binadamu na viongozi mbalimbali kutoka taasisi tofauti nchini.
Amesema baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya ndoa inayotumika sasa vinakiuka na kukandamiza haki za wanawake hasa wale wa wasiokuwa na uelewa wa masuala ya sheria ya ndoa.
Kwa upande wa kuwasaidia wanawake kisheria amesema serikali isiwaache wanaharakati wenyewe katika kufichua na kutatua matatizo ya unyanyasaji wa kijinsia bali wawawezeshe wanasheria hao wanaotoa msaada wa kisheria kwa wanawake wahanga wa vitendo vya ukatili kwakuwa wanawake wengi hasa wale wa vijijini hawajui haki zao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu ambaye pia ni Mkurugenzi Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi.Tike Mwambipile amependekeza kuundwa kwa kitengo kinachoratibu masuala ya familia katika Mahakama kuu.
Previous
Next Post »