MAJAMBAZI YAWACHEZA KWAYA NA KUWAPIGISHA MAOMBI WENYE NYUMBA KABLA YA KUWAIBIA - Rhevan Media

MAJAMBAZI YAWACHEZA KWAYA NA KUWAPIGISHA MAOMBI WENYE NYUMBA KABLA YA KUWAIBIA

Baba wa familia iliyoporwa jana katika mtaa wa Epe mjini Lagos nchini Nigeria, amesimulia kuwa Majambazi waliwaamuru kushiriki nao kucheza kwaya na kumtukuza Mungu kwanza kwa maombi kabla ya kuwapora mali zao.

Bwana huyo aliyefahamika kwa majina ya Michael Oyuma, amesema majambazi hayo licha ya kuwa na silaha mbalimbali lakini pia kila mmoja alikuwa na biblia mkononi.

Amezitaja mali zilizoibiwa kuwa ni pamoja na simu za mkononi, Kompyuta mpakato mashine za mazoezi na za kufulia pamoja na fedha taslimu.

Taarifa inasema Majambazi hao waliendesha Ibada ya dakika 15 ‘Wakinena kwa Lugha’
Previous
Next Post »