Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeendesha operesheni katika maeneo
mbalimbali ya jiji hilo na kuwakamata watuhumiwa 67 wakiwemo watano
waliokutwa wakiuza na kusambaza pombe bandia aina ya konyagi na vifaa
vya kutengeneza kinywaji hicho.
Akizunguma
jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna wa
Polisi, Simon Sirro alisema watuhumiwa hao pia walikamatwa wakiwa na
chupa tupu za konyagi 175, chupa zenye kinywaji cha konyagi 17 na
vifungashio vya viroba vya konyagi 111.
Aidha,
alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na vifuniko vya chupa za
konyagi 200, lebo na stika za konyagi, katoni 111 za viroba vya konyagi,
vimiminika vya pombe aina ya spiriti lita 20, ndoo kubwa aina ya jaba
moja na koki 10, viroba original pakiti 14,916 na Victorious pakiti
1,080.
Aliwataja
watuhumiwa waliokamatwa na bidhaa hizo bandia kuwa ni Ladness Kagaruki
(26), mkazi wa Sinza madukani, Aloyce Emmanuel (53), mkazi wa Salasala,
Leonard Arobogasti (49), mkazi wa Makongo, Godfrey Gabriel (29) na
Eveline Sandole (58) wakazi wa Mwenge.
Kamanda
Sirro alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi
utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili,
huku akieleza kuwa kwa suala la shisha, tayari watuhumiwa watatu
wanashikiliwa na upelelezi wao utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
Katika
tukio lingine, wanamshikilia Kulwa Rajabu anayetuhumiwa kwa ujambazi
akiwa na silaha aina ya Browning yenye namba A731441 yenye risasi 12
ndani ya magazine.
Alisema
mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba 16, mwaka huu saa 10.00 jioni Mbande
Mbagala baada ya kuwekewa mtego. Alisema silaha hiyo iliibiwa Novemba
13, saa 9.30 usiku maeneo ya Tuangoma katika tukio la uvunjaji na kuibwa
kwa vifaa mbalimbali ambavyo vyote vilipatikana.
Aidha,
alisema baada ya mahojiano ya kina mtuhumiwa huyo alitaja silaha
nyingine ambayo ni bastola aina ya Revolver iliyofutwa namba ikiwa na
risasi mbili ikiwa imefichwa maeneo ya msitu wa Dona huko Yombo.
Pia
wamemkamata mtuhumiwa anayetambulika kwa jina moja la Shomari aliyekuwa
akituhumiwa kwa mauaji yaliyofanyika kwenye daladala Oktoba 28, mwaka
huu Tandika Tambuka.
Kwa
mujibu wa Sirro, baada ya Polisi kupata taarifa na kumfuatilia,
mtuhumiwa huyo alianza kukimbia na ndipo askari walifyatua risasi juu
ili asimame, lakini hakutii amri na askari walimpiga risasi mbili mguuni
na kudondoka chini kisha kumkamata pamoja na bastola yake aina ya
Revolver ikiwa na risasi mbili ndani ya magazine.
Sign up here with your email