Kutokana
na mabadiliko ya mafunzo ya ualimu yaliyo fanywa na Wizara ya Elimu
,Sayansi, Tektinolojia na ufundi novemba mwaka huu kuondoa mamlaka ya
usimamizi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Baraza la taifa
elimu ya ufundi NACTE na kuyarudisha wizara ya Elimu chini ya
uangalizi wa baraza la mitihani Tanzana NECTA, shirika lisilo la
kiserikali linalojishughulisha na Elimu nchini (HAKI ELIMU )
limeipongeza Serikali kwa hatua hiyo kwani hapo awali kwa kushirikiana
na wadau wengine wa Elimu lilikuwa limesha toa mapendekezo kama hayo
lakini hayakufanyiwa kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, mkurugenzi mtendaji wa HAKI ELIMU ,Bwana John Kalage alisema
mabadiliko hayo yatasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini,ingawa
mabadiliko ya awali yalikuwa na lengo jema la kukabiliana na upungufu
mkubwa wa waalimu wa kufundisha masomo ya Sayansi katika shule nyingi
hapa nchini lakini yalikuwa na athari ya kuzorotesha ubora wa Elimu.
Alisema ,utaratibu wa kuvifanya vyuo vya elimu kujitegemea katika kudahili wanafunzi,
kutathimini na kutunza waalimu tarajali ulikuwa pia na athali ya
kushusha kiwango mafunzo ya ualimu kwakuwa kila taasisi iikuwa na
uhuru wa kujiamulia viwango vya ubora wa mafunzo itakayo toa ,
“Katika
zama hizi za ushindani kulikuwa na hatari dhahili kuwa kila taasisi
ingeweza kudahili na kufaulisha wanafunzi wake hata wasio stahili ili
kuvutia wana chuo wengi zaidi kwalengo la kujipatia ada ‘’alisema
Hatahivyo
shirika hilo limetoa baadhi ya mapendekezo na kuishauri Serikali
kuunda chombo chenye mamlaka ya juu katika elimu (Education Reguratory
Authority ) chini ya sheria ya elimu ili kusimamia na kulinda sera
,sheria ,kanunu na miongozo ya elimu iliyo wekwa ili kupunguza
maamuzi na mabadiliko ya mara kwa mara katika secta ya Elimu
“Kwa
sasa ina onekana waziri ana mamlaka makubwa makubwa ya kutoa
maamuzi hali inayo onekana kuwepo kwa nyaraka nyingi zinazo badilika
kia mara hata kabla hazija fanyiwa kazi kikamilifu”
Kalage alisema
nivema mafunzo ya ualimu ngazi zote yakaendelea kutolewa na vyuo
vikuu na vyuo vya ualimu peke yake na vyuo vingine visivyo vya ualimu
visiruhusiwe kutoa mafunzo hayo kwa kuwa lengo lao sikutoa mafunzo hayo .
"Nibora
kuwa na vyuo vichachache ambavyo serikali ina uhakika na uandaaji wake
ili vyuo hivi vilishe shule zote za umma na bnafsi ,hii itasaidia kuboresha kiwango cha elimu nchini."alisema
Sign up here with your email