MKUU wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Juma Irando amepiga marufuku nafaka kutengenezea pombe wilayani humo.
Alisema hatua hiyo itawezesha kutunza chakula cha kutosha na kukabiliana na janga la njaa.
Alikuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Chilulumo Tarafa ya Kamsamba.
Irando alisema wananchi wamekuwa wakitumia nafaka nyingi kutengenezea pombe za kienyeji bila kujali kama wana chakula cha kuwatosha.
Alisema pombe za kienyeji zinatumia nafaka nyingi hususan mahindi na ulezi.
Dc alisema kwa sababu hiyo wananchi wanatakiwa kuacha kutumia nafaka kwa vile hali hiyo inaweza kusababisha baa la njaa kipindi mazao yakiwa hayajakomaa.
“Ni marufuku utengenezaji wa pombe za kienyeji kwa kutumia nafaka.
“Mwaka huu kutokana na taarifa za watalamu wa hali ya hewa, inaonekana mvua itakuwa kidogo na kunaweza kukawa na baa la njaa,” alisema Irando.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Hiyo, Mathew Chikoti, aliwaasa wananchi kuwa na utaratibu wa kuweka akiba ya chakula wakati wa mavuno na kutokuuza ovyo.
Alisema hatua hiyo itawawezesha kukabiliana na baa la njaa wakati mazao mengine bado hayajakomaa.
Alisema wananchi wanatakiwa kulima mazao yanayostahimili ukame na yanayowahi kukomaa kutokana na taarifa ya kutokuwapo kwa mvua ya kutosha.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Momba Adrian Jungu alisema yeye na wataalamu wake watahakikisha wanasimamia pembejeo ziwe katika ubora na wananchi wasipate shida wakati wa msimu wa kilimo.

Sign up here with your email