DC KONGWA,MH.NDEJEMBI ASHIRIKI NA KUHIMIZA UJENZI WA MADARASA KATA YA HOGORO. - Rhevan Media

DC KONGWA,MH.NDEJEMBI ASHIRIKI NA KUHIMIZA UJENZI WA MADARASA KATA YA HOGORO.



DC Deo Ndejembi, leo ameshiriki pamoja na viongozi wa Kata ya Hogoro akiwemo Mhe Diwani Mgata na serikali ya kijiji cha Hogoro katika kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Hogoro. 

Hogoro ni kijiji ambacho DC Ndejembi alibaini ufisadi katika ujenzi wa madarasa, ambapo Mwenyekiti wa Kijiji alikuwa ametafuna kiasi cha shilingi milioni sita za ujenzi. 

Leo DC amefika na kuhamasisha ujenzi ufanywe kwa nguvu za wananchi. Kongwa ina upungufu wa takribani madarasa 231 na wilaya imeweka mkakati wa kumaliza upungufu huo.
 DC Deo Ndejembi,akiweka tofali kwenye msingi ikiwa ni sehemu ya ushiriki wake wa ujenzi akishirikiana pamoja na viongozi wa Kata ya Hogoro akiwemo Mhe Diwani Mgata na serekali ya kijiji cha Hogoro katika kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Hogoro. Wilaya ya Kongwa ina upungufu wa takribani madarasa 231 na wilaya imeweka mkakati wa kumaliza upungufu huo.
 DC Deo Ndejembi,akishriki kuchimba msingi ikiwa ni sehemu ya ushiriki wake wa ujenzi akishirikiana pamoja na viongozi wa Kata ya Hogoro akiwemo Mhe Diwani Mgata na serekali ya kijiji cha Hogoro katika kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Hogoro. Wilaya ya Kongwa ina upungufu wa takribani madarasa 231 na wilaya imeweka mkakati wa kumaliza upungufu huo.


Previous
Next Post »