Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Nyamihaga Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amekufa baada ya kunajisiwa na baba yake wa kambo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kwamba
wamemtia mbaroni mtuhumiwa Hamimu Saidi (27) mkazi wa kijiji hicho cha
Nyamihaga.
Akitoa
maelekezo kuhusu mkasa huo, Kamanda Mtui alisema mtuhumiwa alitekeleza
dhamira yake hiyo wakati mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mke wa
mtuhumiwa alipokwenda kisimani kuchota maji.
Alisema
baada ya mwanamke huyo kurejea nyumbani kutoka kisimani alimshuhudia
mtoto wake akilalamika sana wakati akitaka kujisaidia haja ndogo na
ndipo alipomchunguza akagundua kwamba mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na
kujeruhiwa kwenye sehemu zake za siri.
Kamanda
Mtui alisema baada ya kugundua hilo, mama huyo wa mtoto alimchukua
mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Maweni kwa matibabu, ambako
iligunduliwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na alikuwa amebanwa
shingo wakati akifanyiwa kitendo hicho hivyo alikosa pumzi wakati
akifanyiwa unyama huo.
Kamanda
huyo alisema hata hivyo mtoto huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa
ya Maweni alipokuwa akitibiwa na kwamba baada ya uchunguzi wa kidaktari
na uchunguzi wa Polisi, mwili wa mtoto huyo ulikabidhiwa kwa ndugu kwa
ajili ya maziko.
“Kwa
sasa mtuhumiwa Hamimu Saidi anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
mjini Kigoma wakati upelelezi ukiendelea ili taratibu za kumfikisha
mahakamani zifanyike na kwamba anatarajia kufikishwa mahakamani wakati
wowote upelelezi huo utakapokamilika,” alieleza Kamanda Mtui.
Sign up here with your email