Menejimenti ya TTCL na TANROADS wakiwa katika hafla ya kusaini mkataba wa TTCL kutoa huduma ya intaneti na kuuganisha ofisi za TANROADS nchi nzima kupitia Mkongo wa TTCL.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura (Kulia), Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfungale (Katikati) na Mwanasheria wa TANROADS Dora Komba (Kushoto) wakisaini mkataba wa makubaliano ya TTCL kutoa huduma ya kuunganisha ofisi za TANROADS nchi nzima.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani baada ya TTCL kupata zabuni ya kuuganisha ofisi za TANROADS nchi nzima kwenye mkongo wa TTCL.
WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL zimetiliana saini Mkataba wa huduma za Intaneti ambapo TTCL itaunganisha ofisi za Wakala hiyo nchi nzima kwa kutumia Mkongo wake wa Mawasiliano.
Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na kuhudhuriwa na Mtendaji Mkuu (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, Afisa Mtendaji Mkuu (TTCL), Dkt Kamugisha Kazaura pamoja na maafisa Waandamizi kutoka TTCL na TANROADS.
Mradi huo utakaotekelezwa katika Mikoa 25 na Vituo (3) vya mizani utatumia miundombinu ya mawasiliano ya Kampuni ya TTCL iliyounganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB). Mikoa hiyo ni pamoja Makao Makuu ya TANROADS, Mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma, Tanga, Mtwara, Kibaha, Iringa, Musoma na Bukoba.
Mikoa mingine ni Dar es salaam(Keko na Mabibo), Lindi, Makambako, Mwanza, Songea, Manyara, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Sumbawanga, Simiyu(Bariadi), Arusha, Mpanda, Moshi, Geita na Morogoro
Kampuni ya Simu Tanzania TTCL inatekeleza Mpango Mkubwa wa Mageuzi ya Kibiashara ambao umelenga kuboresha miundombinu ya Mtandao na biashara ili kukidhi mahitaji ya wateja na Nchi katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasilaino. Hadi sasa, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeunganisha makampuni binafsi, Mashirika ya Umma na ofisi za serikali zaidi ya 80 kwenye miundombinu ya mawasiliano ya TTCL yenye ufanisi mkubwa wa kimawasiliano ndani na nje ya nchi.
Sign up here with your email