Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo
pichani) wakati wa ufungaji mafunzo kwa askari na maafisa hao
yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi.
Askari na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika
matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi
waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya
kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na
Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akitizama matundu ya risasi zilizolengwa na mmoja wa askari wa uhifadhi
waliohitimu mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.Kulia
kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan
Kijazi.
Sign up here with your email