SIRRO- CHADEMA WANAHONGA VIJANA ILI WAANDAMANE - Rhevan Media

SIRRO- CHADEMA WANAHONGA VIJANA ILI WAANDAMANE

Tokeo la picha la POLISI Kanda ya Dar es Salaam

POLISI Kanda ya Dar es Salaam imekituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwalipa fedha kiasi cha Sh 40,000 baadhi ya vijana ili washiriki katika maandamano ya Ukuta ya Septemba Mosi yaliyopigwa marufuku.

Aidha, imesisitiza imejipanga kikamilifu kukabiliana na watu watakaovunja sheria kwa kufanya maandamano hayo ambayo yamepigwa marufuku kwa lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi.Kauli hiyo ilitolewa  na Kamanda wa Kanda hiyo, Simon Sirro wakati akizungumza jijini Dar es Salaam ambapo alisema, kwa sasa jiji hilo liko shwari na hata baada ya Septemba Mosi, litaendelea kuwa shwari.

“Naomba niwasihi Wana Dar es Salaam hasa vijana wasiingie barabarani hiyo tarehe moja, tuwaachie wachache ambao nia yao ni kuleta fujo, wote tunajua madhara ya fujo, wote tunajua hasara ya fujo, siku hiyo imetolewa katazo hakuna maandamano,” alisema Sirro.

Akizungumzia tuhuma hizo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema, chama hicho hakina fedha za kuwalipa vijana ili kufanya maandamano na kusisitiza; “Tukutane tarehe moja Septemba.”

Previous
Next Post »