Mtendaji Mkuu wa mradi wa mabasi hayo, Ronald Rwakatare amewaeleza wajumbe wa kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa waliotembelea mradi huo kuwa wanatarajia mabasi hayo yataanza kazi Aprili mwakani.
Rwakatare amesema kuwa tayari serikali imeshatangaza zabuni ya kununua mabasi hayo na mwezi Disemba, mwaka huu itasaini mkataba na mzabuni huyo.
“Mabasi haya yatahudumia maeneo ya Morocco, Tegeta, Masaki, Makumbusho na mengine yasiyofikiwa, wakati tukiendelea na ujenzi wa awamu ya pili ya mradi huo,” amesema mtendaji huyo. Mradi wa ujenzi wa barabara wa awamu ya pili unatarajiwa kuhusisha maeneo yenye wakazi wengi na yenye shida ya usafiri ambapo ni kati ya Mbagala na Gongo la Mboto.
Sign up here with your email